Thursday, March 24, 2016
Wednesday, March 23, 2016
Friday, March 18, 2016
Thursday, March 17, 2016
Wednesday, March 16, 2016
Mkuu Mpya Wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu Atoa Onyo Kali Kwa Majambazi na Wahalifu.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa Kijuu amewataka
watu wote wanaopindisha sheria, majambazi na wahalifu wote kutafuta kazi
nyingine halali za kufanya.
Meja
Kijuu aliyasema hayo baada ya kula kiapo cha utiifu na uadilifu
kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Kagera mkoa ambao upo pembezoni mwa nchi
unaokabiliwa na matukio ya mara kwa mara ya uhalifu.
''Namshukuru
Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu na nitafanya kazi kwa
kuzingatia yale ambayo ameyasema na kuhakikisha maendeleo
yanapatikana''-Amesema Meja Kijuu
''Sitakubali
watu wazurure hovyo na kuacha kufanya kazi za uzalishaji na
nitahakikisha napambana na wahalifu wote kwa uwezo wote nilionao"-Amesisitiza Meja Kijuu.
Aidha
Rais Magufuli aliwaapisha wanajeshi wastaafu Meja Jenerali Mstaafu,
Ezekiel Elias Kyunga, aliyekuwa Chuo cha Kamanda na Unadhimu (JWTZ)
ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Jenerali Mstaafu Salum Mustafa
Kijuu, aliyekuwa Mkuu wa Kamandi ya Nchi Kavu ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Wengine
ni Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa(JKT) sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Brigedia Jenerali
Mstaafu Emmanuel Maganga, aliyekuwa Makao Makuu ya Jeshi sasa ni Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma
Lengo la Rais kuweka wanajeshi katika mikoa ya pembezoni ni kuleta usalama na kuimarisha amani katika mikoa hiyo.
Lengo la Rais kuweka wanajeshi katika mikoa ya pembezoni ni kuleta usalama na kuimarisha amani katika mikoa hiyo.
Wednesday, March 16, 2016
Rais Magufuli Akagua Na Kuweka Jiwe La Msingi Katika Ujenzi Wa Kituo Cha Kufua Umeme wa Megawat 240 Cha Kinyerezi II Jijini Dar Es Salaam Marchi 16,2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa
wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria
uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida , Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba
wakivuta utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua
umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi
John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja
wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi John Mageni akitoa
maelekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli kuhusu mitambo ya kufua umeme kwa kinyerezi I nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi wa kinyerezi hawapo pichani kabla ya kuzindua
rasmi Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi
mkuu wa Tanesco Felchesmi Mramba akifafanua jinsi ujenzi wa Kituo cha
kufua umeme cha Kinyerezi II kitakavyokuwa mara baada ya kukamilika
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam CCM
Ramadhani Madabida kabla ya uzinduzi wa uzinduzi rasmi wa Ujenzi wa
Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan
Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
,Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha
Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na
utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya
uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akimkaribisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati
alipowasili kwenye ofisi za kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I
nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Wananchi
wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia huko Kinyerezi nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam
Thursday, March 17, 2016
Rais Magufuli Apiga MARUFUKU Kukodi Mitambo ya Kuzalisha Umeme
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe
16 Machi, 2016 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa kuzalisha
umeme wa Kinyerezi namba mbili, uliopo katika wilaya ya Ilala Mkoani Dar
es salaam, ambao utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha
megawatts 240 za umeme.
Mradi
huo ambao utazalisha umeme kwa kutumia gesi asilia inayosafirishwa kwa
bomba kutoka Mtwara, unatarajiwa kuanza kuzalisha umeme katika kipindi
cha kuanzia miezi 21 hadi 28 utakapokamilika kabisa.
Kuanza
kwa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme huo, kunafuatia juhudi
zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano ya kufanikisha upatikanaji wa
shilingi bilioni 120, ikiwa ni asilimia 15 ya fedha zilizopaswa kutolewa
na Tanzania na fedha nyingine shilingi Bilioni 292 zimetolewa na Japan.
Mradi
huu umetanguliwa na mradi wa Kinyerezi namba moja ambao una uwezo wa
kuzalisha megawatts 150 za umeme, na mitambo yake tayari imeanza
uzalishaji wa megawatts 105 zilizoingizwa katika gridi ya Taifa.
Pamoja
na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Kinyerezi namba mbili,
Rais Magufuli amekagua mitambo ya kuzalisha umeme ya mradi wa Kinyerezi
namba moja, ambapo Mkuu wa Kituo cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
cha Kinyerezi Mhandisi John Mageni, ametoa maelezo kuwa shirika hilo
lina mpango wa kupanua uzalishaji wa umeme katika mradi huo kutoka
megawatts 150 hadi kufikia megawatta 335, kwa kuongeza mitambo ya kufua
umeme kwa teknolojia inayojumuisha matumizi ya gesi asilia na mvuke
uzalishwao na mitambo hiyo.
Baadaya
ya kupokea maelezo hayo, Rais Magufuli ameridhia kuwa serikali yake
itatoa Dola za kimarekani milioni 20, kwa ajili ya kufanikisha upanuzi
wa mradi huo na ameagiza kuwa wataalamu wa TANESCO washirikiane na
Mkandalasi kuhakikisha upanuzi huo unafanyika haraka iwezekanavyo,
badala ya muda wa miezi 12 uliopangwa.
Akizungumza
na wananchi waliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huo, Rais
Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini na
TANESCO, kuanza kuachana na mitambo ya kukodi kwa ajili ya kuzalisha
umeme, na badala yake nchi ijenge mitambo yake yenyewe ili kuondokana na
gharama kubwa za nishati hiyo muhimu.
“Waziri,
ukiona mtaalamu anakuletea mapendekezo ya kutaka kukodi mitambo ya
kuzalisha umeme, badala ya kuleta mapendekezo ya kununua mitambo yetu
wenyewe ujue mtaalamu huyo hafai, mtoe” Amesisitiza Rais Magufuli
Ameongeza
kuwa tafiti zimethibitisha kuwa hadi sasa Tanzania ina zaidi ya futi za
ujazo Trilioni 57 za gesi asilia, ambayo itazalisha umeme wa
kutosheleza mahitaji ya ndani, na umeme mwingine kuuzwa nje ya nchi
ikiwemo Kenya ambayo tayari imeomba kuuziwa umeme kutoka Tanzania.
Aidha,
Rais Magufuli ametoa onyo kwa TANESCO kuwa hatarajii kusikia bwawa la
maji la Mtera limeishiwa maji, kwa kuwa katika msimu huu wa mvua maeneo
ya Iringa yalikuwa na mvua nyingi ambazo zimesababisha hadi mafuriko
mafurukio.
Kwa
upande wake, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema
tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, juhudi zilizofanyika
zimefanikisha kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawatts 800 hadi
kufikia megawatts 1,000 kiasi ambacho ni pungufu kwa megawatts 20 tu,
ikilinganishwa na mahitaji ya megawatts 1020 za sasa.
Ameongeza
kuwa pamoja na kuweka jiwe la msingi la mradi wa Kinyerezi namba mbili,
hivi karibuni serikali inatarajia kujenga miradi mingine ya kuzalisha
umeme kwa kutumia gesi asilia, ikiwemo Kinyerezi namba tatu
utakaozalisha megawatts 600, Kinyerezi namba nne utakaozalisha megawatts
300, na mingine itakayojengwa Lindi na Mtwara.
Prof.
Muhongo amebainisha kuwa mpaka sasa gesi asilia inazalisha kati ya
asilimia 50 na 60 ya umeme wote hapa nchini, Maji yanazalisha asilimia
30 hadi 40, na umeme unaozalishwa kwa mafuta hauvuki asilimia 10.
Sherehe
hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa Japani
hapa nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida, Wabunge wa kamati ya Nishati na
Madini, wafadhili wakiwemo Benki ya Dunia, Benki ya Afrika na Shirika
misaada la Japan (JICA.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Machi, 2016
Rais Magufuli Akerwa Na Mikataba Mibovu Ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL....Aeleza Kilichomfanya Amrudishe Profesa Muhongo Wizara ya Nishati
Rais John Magufuli jana aliitaja
kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL wakati akizungumzia matatizo
yanayosababishwa na kununua umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi na
kupiga marufuku mikataba hiyo.
Rais pia alipuuzia shutuma zinazorushwa
dhidi ya Profesa Sospeter Muhongo, ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri
wa Nishati na Madini kutokana na sakata la IPTL, akisema “wakati
mwingine vitu vizuri hupigwa vita” na hivyo amemrejesha mbunge huyo
wa Musoma Vijijini kwenye wizara hiyo kwa sababu ya uchapakazi na si siasa.
Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli amekuwa akifichua kashfa za
ufisadi ambazo hazikuwahi kujadiliwa vikali katika utawala uliopita,
lakini jana alitoa mfano wa IPTL kama moja ya mikataba iliyoisababishia
Serikali matatizo.
Kashfa zilizoikumba sekta hiyo ni pamoja na mkataba
wa uzalishaji umeme na kampuni ya Richmond Development iliyodhihirika
baadaye kuwa haikuwa na uwezo, uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni
kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyohusisha IPTL, mikataba ya
ununuzi umeme kwa bei kubwa kutoka kampuni binafsi na ununuzi wa umeme
kutoka mitambo ya kukodi.
“Ni matumani yangu kuwa sitasikia tena mnaleta mapendekezo kwamba tunataka kuongeza mkataba huu au tunataka kukodi mtambo huu.Suala la kukodi likalegee, lizimie na life kabisa huko,” alisema Rais Magufuli wakati akizindua ujenzi wa kituo cha umeme cha mradi wa Kinyerezi ll utakaokuwa ukizalisha megawati 280 kwa mwaka jijini Dar es Salaam jana.
“Ni matumani yangu kuwa sitasikia tena mnaleta mapendekezo kwamba tunataka kuongeza mkataba huu au tunataka kukodi mtambo huu.Suala la kukodi likalegee, lizimie na life kabisa huko,” alisema Rais Magufuli wakati akizindua ujenzi wa kituo cha umeme cha mradi wa Kinyerezi ll utakaokuwa ukizalisha megawati 280 kwa mwaka jijini Dar es Salaam jana.
“Hayo mawazo yafe, sasa tuwe na mawazo ya
kujenga mitambo yetu. Cha kuazima ni kibaya. Hivi sasa vya kukodi na vya
kuazima achaneni navyo. Nendeni na mawazo ya kujenga mitambo yetu.
“Tumechoka kuchezewa. Kuna miradi hapa ya hovyo kweli. Kila siku inazaa matatizo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri (Muhongo) lisimamie hilo. " Alisema Rais Magufuli
Alisema Profesa Muhongo akipata ushauri kutoka kwa wataalamu wake kuhusu miradi ya kukodi mitambo, atambue kuwa hawafai. “Ujue huyo si mtaalamu mzuri, ikiwezekana mtoe. Wataalamu wako wakuletee mawazo ya kujenga mitambo yetu,” alisema.
“Tumechoka kuchezewa. Kuna miradi hapa ya hovyo kweli. Kila siku inazaa matatizo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri (Muhongo) lisimamie hilo. " Alisema Rais Magufuli
Alisema Profesa Muhongo akipata ushauri kutoka kwa wataalamu wake kuhusu miradi ya kukodi mitambo, atambue kuwa hawafai. “Ujue huyo si mtaalamu mzuri, ikiwezekana mtoe. Wataalamu wako wakuletee mawazo ya kujenga mitambo yetu,” alisema.
Rais Magufuli alisema ni lazima ufike wakati Tanzania
iwe na umeme wa uhakika tena wa kujitegemea.
“Si umeme kwa kukodisha- kodisha. Umeme ni wa kutumia watu. Na ndiyo maana kumekuwa na matatizo mengi. Mara IPTL mara nini. Ni kwa sababu tulizoea umeme wa kukodisha kwa wafanyabiashara,” alisema.
“Si umeme kwa kukodisha- kodisha. Umeme ni wa kutumia watu. Na ndiyo maana kumekuwa na matatizo mengi. Mara IPTL mara nini. Ni kwa sababu tulizoea umeme wa kukodisha kwa wafanyabiashara,” alisema.
Kampuni ya IPTL iliingia kwenye mgogoro
na Serikali baada ya kudaiwa kuwa inaitoza Tanesco tozo kubwa gharama za
uwekezaji kuliko makubaliano ya mkataba.
Wakati wa kashfa ya escrow,
zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa zimewekwa kwenye akaunti hiyo kusubiri
kumalizika kwa mgogoro wa kimkataba baina ya IPTL na Tanesco zilichotwa
na kuonekana zikiingia kwenye akaunti za mawaziri, majaji, wabunge na
watumishi waandamizi wa Serikali, jambo lililolifanya Bunge limlazimishe
Profesa Muhongo awajibike kwa kushindwa kusimamia fedha za Serikali.
Profesa Muhongo alijiuzulu, lakini akateuliwa na Rais Magufuli kurudi
kwenye nafasi hiyo na jana mkuu huyo wa nchi hakusita kummwagia sifa.
“Wizara ya Nishati mmenifurahisha sana. Tuachane na mitambo ya kukodi. Tumechoka kufanya biashara na wawekezaji wa ajabu ajabu. Halafu tunalipia capacity charges za ajabu na umeme unakuwa juu. Tunawapa shida Watanzania wa maisha ya chini,” alisema Magufuli.
“Wizara ya Nishati mmenifurahisha sana. Tuachane na mitambo ya kukodi. Tumechoka kufanya biashara na wawekezaji wa ajabu ajabu. Halafu tunalipia capacity charges za ajabu na umeme unakuwa juu. Tunawapa shida Watanzania wa maisha ya chini,” alisema Magufuli.
“Nendeni kwa kasi ya
hapa kazi tu. Na ndiyo maana niliamua kumrudisha Profesa Muhongo hapo.
Wakati mwingine vitu vizuri vinapigwa vita. Sichagui mwanasiasa. Mimi
nataka mtu mchapa kazi. Maendeleo hayana chama.”
Akizungumzia ujenzi wa
kituo cha Kinyerezi ll utakaogharimu dola 344 za Marekani (sawa na Sh688
bilioni), Rais alisema amefarijika kuona ndani ya muda wake mfupi akiwa
madarakani amealikwa kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.
Alisema
Serikali ya Japan ilitoa dola 292 milioni za Marekani na Tanzania
ilitakiwa kutoa dola 52 milioni za Marekani sawa na asilimia 15, lakini
ikashindikana na kutakiwa wasubiri.
“Baada ya makusanyo kuimarika
tulipoingia madarakani mwezi Novemba na Desemba mwaka jana, tulitoa
maelekezo na hizo dola 52 milioni sawa Sh110 bilioni za Tanzania na
zikapatikana ndiyo maana leo tupo hapa kuweka jiwe la msingi kwa ajili
ya mradi huu kuanza,” alisema.
“Hivi sasa tuna uwezo wa kuzalisha
megawati 1,200 hadi 1,500 za umeme kwa mwaka. Sasa tumefikia 1026. Hiyo
ina maana kuwa kila Mtanzania kwa sasa anatumia wastani wa wati 30 kwa
mwaka,” alisema.
Pia alisema amefurahi kupata taarifa kuwa mradi ya
Kinyerezi l utaongezewa uwezo wa uzalishaji kutoka megawati 150 hadi
335.
“Nimeambiwa mkandarasi anataka dola 20 milioni za Marekani (sawa
na Sh 40 bilioni). Sasa kama tuliweza kutoa hela kwa ajili ya Kinyerezi
II, hatuwezi kushindwa kuongeza kwa ajili ya Kinyerezi l. Hiyo hela
tutatafuta hata mwezi huu tutampa,” alisema.
Kiongozi wa CUF Aliyetangaza Kuwa Wafuasi wa Chama Hicho Wamekimbilia Porini Akamatwa na Polisi
Ikiwa ni siku tatu tangu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad, atangaze kuwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar wanakimbilia porini kuhofia usalama wao, ametiwa mbaroni.
Kukamatwa
kwa Masoud sasa kunafanya idadi ya viongozi wa chama hicho waliotiwa
mbaroni na kuhojiwa polisi kufikia wanne tangu kufutwa kwa matokeo ya
Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka jana.
Viongozi
wengine waliohojiwa na Polisi na kuachiwa kwa dhamana ni Naibu Katibu
Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Alin
Shehe na mshauri wa mikakati wa chama hicho, Eddy Riyami.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, jana
alithibitisha kukamatwa kwa Masoud, ambaye ni Waziri wa zamani wa
Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Alisema kiongozi huyo alikamatwa na kitengo cha upelelezi nyumbani kwake mtaa wa Mbweni mjini Zanzibar jana.
Alisema
kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ili
kusadia uchunguzi juu ya taarifa alizotoa katika mkutano wake na
waandishi wa habari na kuzungumzia hali ya amani ya Zanzibar na wananchi
wake.
“Tunamshikilia
kwa uchunguzi, kuna mambo ya msingi tunaona yanahitaji kufanyiwa
uchunguzi na yeye kusadia polisi uchunguzi wake,” alisema Mkadam.
Kufuatia
kukamatwa huko kwa Masoud, CUF imelaani kitendo hicho na kusema kuwa
kamata kamata hiyo inawalenga viongozi wa chama hicho na wanachama wake
pekee.
Naibu
Katibu Mkuu wa chama hicho, Mazrui alisema matukio yote ya uvunjifu wa
amani yaliyotokea visiwani hapa, yamekuwa yakihusishwa na CUF na Jeshi
la Polisi huwakamata viongozi wa chama hicho pekee.
“Tunasema
huu ni uonevu wa hali ya juu, maana viongozi na wafuasi wa CUF pekee
ndio wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi, hii yote inatokana na uchaguzi
wa marudio, hivyo kutoshiriki kwetu kwa uchaguzi isiwe sababu ya
kuadhibiwa,” alisema.
Aidha,
alisema suala la kushiriki au kutoshiriki katika uchaguzi ni hiari ya
mtu, hivyo kwa wale ambao hawatashiriki uchaguzi huo, wasiadhibiwe wala
wasidhalilishwe na wale ambao wametangaza kushiriki waende wakapige
kura.
Kwa
upande wa mke wa Masoud, Rahma Issa, alisema askari kazu wasiopungua
sita wakiwa na silaha za moto mbili walifika nyumbani jana saa moja
asubuhi na kudai wanamhitaji mumewe.
Alisema
baada ya kubisha hodi, kijana wake mmoja alifungua mlango na kisha
askari watatu waliingia ndani mmoja akiwa na silaha ya moto kifuani.
“Baada ya kuamshwa na kutoka chumbani walimwambia yupo chini ya ulinzi anahitajika kituo cha polisi,” alisema Rahma.
Hata
hivyo, alisema baada ya kumkamata, hawakumwambia sababu ya kukamatwa
kwake, lakini baada ya kuwauliza wanampekeka kituo gani walimwabia Kituo
cha Polisi Mwembe Madema, Zanzibar.
Naye
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema
vitendo vya kukamatwa viongozi wa CUF ni mwendeleo wa Serikali ya CCM
kuwanyanyasa viongozi na wanachama wake chama hivyo visiwani hapa.
Alisema vitendo vnavyoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi vinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na haki za binadamu.
Shehe
alisema matunda ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya kujenga amani na
umoja wa kitaifa yameanza kuvurugwa tangu kuingia mgogoro wa uchaguzi
mkuu.
Subscribe to:
Posts (Atom)