Ajali Mbaya Iliyohusisha Daladala na Malori Mawili Yaua Watu 4 na Kujeruhi 25 Jijini Dar es Salaam
Ajali
Mbaya imetokea leo asubuhi eneo la Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam
ikihusisha malori mawili na daladala iliyo kuwa ikitokea Gongo la Mboto
kuelekea Ubungo
Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali ya Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25 wakijeruhiwa.
Inaelezwa
kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo
liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma,
hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na
Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu
Mnadani.
==
No comments:
Post a Comment