Friday, March 4, 2016
Naibu Waziri wa Afya Dr Kigwangala Azindua Wodi Mpya Ya Wagonjwa Mahututi Muhimbili.....Kasema Serikali ina Mpango wa Kuacha Kupeleka Wagonjwa Nje ya Nchi Kutibiwa
Serikali
imesema ina mpango wa kusitisha kupeleka wagonjwa nje ya nchi kupatiwa
matibabu na kuhakikisha kila kitengo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH) kinakuwa na chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum
(ICU).
Serikali imechukua uamuzi huo, wakati taarifa ndani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto zikieleza inadaiwa deni la Sh.28.74 bilioni za malimbikizo kutokana na ongezeko la wagonjwa wanaopelekwa nje kwa matibabu.
Akizungumza
jana wakati wa kuzindua chumba cha ICU kilichopo jengo la Mwaisela
hospitalini hapo, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk Hamis Kigwangalla
alisema lengo la Serikali ni kuanzisha vyumba hivyo kwa kila kitengo ili
kupunguza vifo.
Alisema
hospitali hiyo ina vitanda 25 vya ICU, lakini lengo ni kuwa na vitanda
150 vya wagonjwa mahututi na wataalamu wa kutosha.
Alisema Serikali ina mpango wa kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi watakaokuwa wamebobea katika fani ya vyumba hivyo.
Madaktari
na wauguzi hao watapata mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Cairo na mengine
yatatolewa kupitia Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (Muhas).
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Mseru alisema kuzinduliwa
kwa ICU hiyo kunaifanya hospitali hiyo kuwa na vyumba vya aina hiyo
viwili vyenye vitanda 25, kutoka chumba cha awali kilichokuwa na vitanda
vinane.
Alisema uwapo wa vitanda hivyo ni ongezeko la asilimia 200 ikilinganishwa na uwezo wa awali.
“Fedha
za ndani zilizotumika kwa ajili ya ukarabati wa chumba hiki ni Sh230
milioni ikiwa ni pamoja na kutafuta ufadhili kutoka taasisi isiyo ya
kiserikali ya Ujerumani iliyowekeza vifaatiba vya Sh600 milioni.
‘‘Mfadhili huyu ndiye aliyetununulia vifaa vyenye thamani ya Dola 800,000 za Marekani,” alisema Profesa Mseru.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla akisisitiza jambo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa
uzinduzi ya wodi ya ICU ilizopo kwenye Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili(MNH)
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hosptitali ya Taifa ya Muhimbili MNH, Profesa
Lawrence Museru (katikati) akitoa maelezo mafupi jana Jijini Dar es
Salaam kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) wakati wa sherehe za uzinduzi wa
wodi ya ICU iliyopo kwenye jengo la Mwaisela katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili(MNH)
Rais
wa Shirika lisilo la Kiserikali la Madaktari wanaohusika na magonjwa ya
ini na tumbo(Gastrenterology) kutoka Munich Ujerumani(kulia) akiteta
jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa uzinduzi wa ICU Muhimbili.
No comments:
Post a Comment