Tuesday, February 9, 2016

Tuesday, February 9, 2016

Hali ya Mufti Mkuu Abubakar Zuberi Yaimarika Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa Tumbo


Hali ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zuberi ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu inaendelea vizuri.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Neema Mwangomo jana alisema mufti amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete   na alifikishwa  Hospitalini  hapo  juzi. 
Jana, viongozi  mbalimbali  wa  serikali  akiwemo  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walimtembelea  kumjulia hali  Mufti Zeburi

Pia,baadhi ya waumini wa Kiislamu jana mchana walionekana nje ya jengo hilo wakitaka kufahamu maendeleo ya afya ya kiongozi wao huyo. 

Tuesday, February 9, 2016

Watendaji wa Sekta ya Afya waaswa kuota taarifa sahihi juu ya idadi ya wagonjwa wa Kipindupindu


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watendaji wa Serikali na Sekta ya Afya kuwajibika ipasavyo kwa  kutoa taarifa sahihi juu ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu nchini.

Akitoa tamko kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu nchini pamoja na tahadhari ya ugonjwa wa Zika jana  jijini Dar es salaam Mhe. Ummy alisema kuwa watendaji watakaoficha taarifa za wagonjwa katika maeneo yao watawajibishwa.

“Mojawapo wa changamoto katika mapambano ya kudhibiti mlipuko huu wa kipindupindu ni utoaji wa idadi pungufu au kutotoa kabisa taarifa za wagonjwa wa kipindupindu hivyo kupelekea kutokuwa na mafanikio katika mikakati iliyowekwa” alisema Waziri Ummy.

Aidha, alitoa wito kwa sekta nyingine kushirikiana na Wizara kupambana na ugonjwa huo ili kukabiliana  na baadhi ya changamoto zinazowakabili watoa huduma za afya na elimu walioko katika maeneo mbalimbali nchini.
 
“ Jukumu la kupambana na mlipuko wa ugonjwa huu si la Wizara ya Afya pekee  naomba sekta nyingine ikiwemo Maji, Miondombinu, Biashara Elimu na Mazingira tushirikiane kwa pamoja ili kuutokomeza ugonjwa huu”.

Mbali na hayo Mhe. Ummy alieleza kuwa takwimu za kuanzia tarehe 1 hadi 7 februari mwaka huu zinaonyesha kuwa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu imepungua kutoka 459 ya wiki iliyoisha tarehe 31 Januari hadi 258 ambapo ni sawa na punguzo la asilimia 44%.

Hata hivyo Wizara imewatoa hofu wananchi na kuwakumbusha kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Zika pamoja na magonjwa mengine yanayoenezwa na Mbu.
Tuesday, February 9, 2016

Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi Ya Makamu Wa Rais

Tuesday, February 9, 2016

Mbuzi Na Kondoo 200 Wakatwakatwa Mapanga Wakituhumiwa Kuvamia Shamba La Mkulima Huko Mvomero Morogoro



Zaidi ya Mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero Mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu ' 
 
Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai
 
Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.
 
Waziri mwenye dhamana kupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio .

Sunday, February 7, 2016


   


Monday, February 8, 2016

Jaji Damian Lubuva Amtaka ' Lowassa' Aache Kuupotosha Umma


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.

Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.

Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.

Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa chama ambaye aliyapinga matokeo hayo.

“Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.

"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.

Chadema, ambayo iliungana na vyama vitatu kuunda Ukawa, iliitaka NEC kusitisha utangazaji matokeo ikidai kuwa kilichokuwa kikitangazwa ni tofauti na takwimu walizokusanya kutoka majimboni. Lakini NEC ikaendelea kutangaza.

Baadaye, Chadema ililalamika ikidai kituo chao cha kukusanya na kujumlisha matokeo kilivamiwa na polisi na kompyuta kuchukuliwa na hivyo kuvuruga ufuatiliaji wao wa matokeo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma kutoka NEC, Emmanuel Kavishe alisema kuwa Tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na Katiba na kwamba hata siku moja haijawahi kumpendelea au kumuonea mtu yeyote.

Katika uchaguzi wa urais, John Magufuli alipata kura milioni 8.8 huku Lowassa akipata milioni 6.07.