Wednesday, December 30, 2015








MWENEBATO

Wednesday, December 30, 2015


 Mh: Lukuvu Aagiza Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufanya kazi hadi Usiku, Abaini Urasimu Mkubwa Wizarani


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watumishi wa wizara hiyo katika kitengo cha huduma kwa wateja, kufanya kazi hadi usiku ili kuhakikisha wanawahudumia kwa muda wananchi wengi wanaofika katika kitengo hicho na kuondoka bila kupata huduma stahiki.

Waziri Lukuvi alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kitengo hicho na kubaini kuwepo urasimu mkubwa unaopelekea wananchi kushindwa kupata huduma kwa wakati. 

Baada ya kuzungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kitengo hicho, alibaini kuwepo wananchi ambao wamekuwa wakifuatilia hati zao kwa takribani miezi mitatu bila mafanikio lakini alipoagiza wapewe hati hizo zilipatikana mara moja.

“Watu wasirudi bila kuhudumiwa. Na kama ni wafanyakazi watabaki mpaka usiku, tutafanya utaratibu wa hao wafanyakazi wanaobaki mpaka usiku. Wafanyakazi wabaki muda zaidi lakini kila anayekuja katika kituo kile lazima ahudumiwe,” alisema Lukuvi.

Pia, Lukuvi aliagiza kufungwa kwa mitambo itakayosaidia kutoa huduma za kieletroniki. Alisema kuwa uanzishwe mfumo wa kuwasiliana na wananchi wanaohitaji huduma katika kitengo hicho kwa njia ya barua pepe, whatsap, simu na kadhalika.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye pia ni kamishna Mkuu wa ardhi, Dk Moses Kusiluka alisema kuwa katika utoaji wa huduma hukutana na changamoto inayotokana na baadhi ya watu wanaotaka kujipatia hati kwa njia za udanganyifu bila kuwa na nyaraka za kisheria husasan wanapokuja kuwawakilisha watu wengine.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )


Tuesday, December 29, 2015

Kizingiti mazungumzo ya amani Burundi


Mazungumzo ya kujaribu kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa nchini Burundi yamefanyika nchini Uganda.
Hata hivyo washiriki wamekosa kuelewana kuhusu siku ya kuanza kwa mazungumzo kamili.
Majadiliano hayo, yaliyoongozwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, yalikuwa ya kuweka mikakati ya kufanyika kwa mazungumzo ya kina kuhusu mzozo nchini humo.
JanuariMachafuko yalianza Burundi baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania uchaguzi kwa muhula wa tatu.
Alishinda uchaguzi huo uliofanyika Januari.
Mkutano huo uliafikia mazungumzo ya kina yaanze Januari 6 mjini Arusha, Tanzania lakini ujumbe wa serikali ya Burundi umesema hakukuwa na “makubaliano kuhusu tarehe hiyo”.
Msemaji wa afisi ya rais wa Burundi Willy Nyamitwe alitoa taarifa kwa vyombo vya habari baada ya mazungumzo ya leo akipinga tarehe hiyo.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ikulu ya rais wa Uganda mjini Entebbe.
Rais Museveni, aliyeteuliwa na viongozi wa kanda kuongoza mazungumzo hayo, ametoa wito kwa upande wa serikali kutochukua msimamo mkali.
"Wanaweza kuwa wahalifu lakini kwa sababu za kuleta amani wacha watu hawa tuwape kinga ya muda. Hata nyinyi wakati ule mlikuwa mnavunja haki za binadamu (mlipokuwa waasi), kama vile kuua raia wa kawaida,” amesema.
Burundi
Bw Museveni ameitaka serikali ya Burundi kutotoa masharti makali
“Huo ni uhalifu wa kivita hata mkiwa waasi. Mkiwa waasi kuweni waasi wazuri, msiwe waasi wabaya kwa kuwaua raia ambao si askari. Unaweza kutenda uhalifu wa kivita ukiwa serikalini au upande wa upinzani.”
Muungano wa Afrika umesema unapanga kutuma walinda amani 5,000 nchini humo, hatua ambayo imepingwa na serikali ya Burundi.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Burundi Alain-Aime Nyamitwe aliongoza ujumbe wa serikali kwenye mazungumzo hayo.
Awali naibu kwanza wa mwenyekiti wa chama tawala cha CNDD FDD Victor Burikukiye alikuwa ametoa masharti kadhaa ikiwemo kutokubali kukaa katika meza moja na "wauaji waliopanga mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli”.
Kulikuwa pia na wawakilishi kutoka vyama vya upinzani na makundi ya kiraia.

Friday, August 28, 2015

Picha za Mafuriko ya Magufuli Sumbawanga


...
Read More

Magufuli Akataa Mawaziri Wazembe......Asema Serikali Yake Haitakuwa na BlaaBlaa Katika Utendaji Kazi

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema serikali yake ya awamu ya tano haitakuwa na blablabla katika utendaji wa kazi na kuonya kuwa waziri atakayeshindwa kutelekeza majukumu yake, ataondolewa ili kupisha wenye uwezo. Dk.  Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi wilayani Nkasi na Kalambo,

Thursday, June 26, 2014

Balotelli adai kiss la shavuni kutoka kwa Malkia wa Uingerezi kama akiisaidia Italy kuifunga Costa Rica

Baada ya England kutandikwa mabao 2 - 1 na Uruguay, Tim hiyo inaitegemea Italy kuifunga Costa Rica katika mechi ya leo ili wajinasue kwenye siti ya basi la kombe la dunia waliokaa mwisho kabisa
Kutokana na timu hiyo kuiombea Italy kushinda ili waendelee kubaki kwenye mashindano ya kombe la dunia, Balotelli ametoa mpya baadaya kudai kiss la shavuni kutoka kwa Malkia wa Uingereza kama ataisaidia Italy kuifunga Costa Rica.
Hiki ndicho alichoki-tweet Baloteli.

"If we beat Costa Rica I want a kiss, obviously on the cheek, from the Uk Queen"